Benki Inayodaiwa Kuchangia Mauaji wa Kimbari Rwanda.


Ufaransa imeanzisha uchunguzi dhidi ya benki ya BNP Paribas, kufuatia madai kuwa ilihusika na mauaji kimbari nchi Rwanda mwaka 1994, ambapo zaidi ya watu 800,000 waliuawa.
Mashirika matatu ya umma yamepeleka kesi mahakamani dhdi ya benki hiyo, wakiilaumu kwa kupitisha dola milioni 1.3 kwa muuza silaha.
Pesa hizo zilitumiwa kununua silaha na kukiuka azimio la marufuku ya silaha la Umoja wa Mataifa.
Papa Francis aomba msamaha kwa mauaji Rwanda
UN: Huenda Sudan Kusini ikakumbwa na mauaji ya kimbari
UN: Kuna hofu ya kutokea mauaji ya kimbari Sudan Kusini
Kanali wa kabila la Hutu ambaye alipokea silaha hizo, Theoneste Bagosora, anatumikia kifungo cha miaka 35 jela kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu.
Mauaji ya kimbari nchini Rwanda yalizuka baada ya ndege iliyokuwa imembeba Rais Juvenal Habyarimana kutoka kabila la Hutu ilidunguliwa Aprili tarehe 6 mwaka 1994.
Wanamgambo wa Hutu kisha wakawaua watu wa Tutsi walio wachache katika kipindi cha siku 100.

Source: Udaku.