Awataskia harufu yake, na kwa hakika harufu yake husikika umbali kadha wa kadhaa)).

Assalam Aleykum warahmatullah wabarakatuh Ndugu zangu katika Imani.

Naam leo nawageukia wale Dada zangu, Mama zangu, Shangazi zangu, Wadogo zangu na Wale wote ambao ni wanawake kuhusu Stara.

Yaani katika zama hizi baadhi ya wanawake mmeamua kuziba masikio kabisa kwa Pamba zenu ili msisikilize yale ambayo mnakumbushwa kuhusu kuwa na Stara au Hijabu.

Enyi dada zangu nawakutumbusha tena kuwa Allaah (Subhannah Wa Ta’ala) atawahukumu kwa yale mnayoyapuuza.

Enyi dada zangu katika Imani na hata Mtume wetu Muhammad (Swalla Allahu ‘Aleyhi wa Sallaam) aliwausia na kuwapa onyo wanawake Wanaovaa Nguo Lakini Wako Uchi Wenye Vichwa Vya Manundu Hawatoingia Peponi Wala Kuisikia Harufu Yake

AL-HADITH

👈عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه) قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((صِنْفَانِ مِنْ أَهْلِ النَّارِ لَمْ أَرَهُمَا: قَوْمٌ مَعَهُمْ سِيَاطٌ كَأَذْنَابِ الْبَقَرِ يَضْرِبُونَ بِهَا النَّاسَ, وَنِسَاءٌ كَاسِيَاتٌ عَارِيَاتٌ مُمِيلاَتٌ مَائِلاَتٌ رُءُوسُهُنَّ كَأَسْنِمَةِ الْبُخْتِ الْمَائِلَةِ, لاَ يَدْخُلْنَ الْجَنَّةَ وَلاَ يَجِدْنَ رِيحَهَا, وَإِنَّ رِيحَهَا لَيُوجَدُ مِنْ مَسِيرَةِ كَذَا وَكَذَا)) مسلم
Maana yake ni
“Imepokelewa kutoka kwa Abu Hurayrah(رضي الله عنه) kwamba Mtume wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم ) amesema: ((Aina mbili za watu wa motoni sijawaonapo [hawapo katika zama zangu]: Watu walio na mijeledi mfano wa mikia ya ng’ombe wanawapiga watu kwa mijeledi hiyo [kwa dhulma], na wanawake waliovaa nguo na ilhali wako uchi, wakitembea kwa maringo huku wakiyanyonga mabega yao na wakiwafunza wengineo kutenda kama hivyo, vichwa vyao ni kama nundu za ngamia-bukhti wanaodemadema. Hawatoingia Peponi wala hawataisikia harufu yake, na kwa hakika harufu yake husikika umbali kadha wa kadhaa)).
Imepokelewa na Imam Muslim

Ndugu zangu katika Imani neno Ngamia bukhti maana yake ni aina ya ngamia wenye shingo ndefu.

Ndugu zangu Hadithi hiyo ni Haramisho kwa wanawake kutokuvaa vazi la Hijaab Aliloamrisha Allaah (سبحانه وتعالى) lenye sitara na heshima.

Ndio maana Allaah (Subhannah Wa Ta’ala) akasema :-
👈 وَقُل لِّلْمُؤْمِنَاتِ يَغْضُضْنَ مِنْ أَبْصَارِهِنَّ وَيَحْفَظْنَ فُرُوجَهُنَّ وَلَا يُبْدِينَ زِينَتَهُنَّ إِلَّا مَا ظَهَرَ مِنْهَا ۖ وَلْيَضْرِبْنَ بِخُمُرِهِنَّ عَلَىٰ جُيُوبِهِنَّ ۖ وَلَا يُبْدِينَ زِينَتَهُنَّ إِلَّا لِبُعُولَتِهِنَّ أَوْ آبَائِهِنَّ أَوْ آبَاءِ بُعُولَتِهِنَّ أَوْ أَبْنَائِهِنَّ أَوْ أَبْنَاءِ بُعُولَتِهِنَّ أَوْ إِخْوَانِهِنَّ أَوْ بَنِي إِخْوَانِهِنَّ أَوْ بَنِي أَخَوَاتِهِنَّ أَوْ نِسَائِهِنَّ أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُنَّ أَوِ التَّابِعِينَ غَيْرِ أُولِي الْإِرْبَةِ مِنَ الرِّجَالِ أَوِ الطِّفْلِ الَّذِينَ لَمْ يَظْهَرُوا عَلَىٰ عَوْرَاتِ النِّسَاءِ ۖ وَلَا يَضْرِبْنَ بِأَرْجُلِهِنَّ لِيُعْلَمَ مَا يُخْفِينَ مِن زِينَتِهِنَّ ۚ
Maana yake ni
“Na waambie Waumini wanawake wainamishe macho yao (wasitazame yaliyoharamishwa kwao), na wahifadhi tupu zao, na wala wasidhihirishe mapambo yao (miili yao) isipokuwa yale yanayodhihirika (kwa kuwa hakuna njia ya kuyaficha). Na waangushe khimaar (shela, ushungi) zao mpaka vifuani mwao, na wasidhihirishe mapambo yao isipokuwa kwa waume zao, au baba zao, au baba za waume wao, au watoto wao wa kiume, au watoto wa kiume wa waume zao, au kaka zao, au watoto wa kiume wa kaka zao, au watoto wa kiume wa dada zao, au wanawake wao (dada zao wa Kiislamu), au wale iliyowamiliki mikono yao ya kuume, au wafuasi wanaume wasio na matamanio (kwa wanawake) miongoni mwa wanaume au watoto ambao hawaelewi (kitu kuhusu) yanayohusu uke. Na wala wasipige miguu yao (wanapotembea; kwa kutaka) yajulikane yale wanayoyajificha katika mapambo yao.
Hiyo ni Suraatul An-Nuwr Aya ya 31

story@moodyhamza