Mwakyembe Kukataza Wasanii Kuimba Siasa

KAULI ya Mwakyembe Kukataza Wasanii Siasa Yazidi Kupigwa…Afande Sele Amshukia Kwa Mfano wa Bob Marley
Afande Sele, Siasa
Afande Sele amesema hayo baada ya siku moja kupita tangu Dkt. Mwakyembe kutoa kauli yake mbele ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwataka wasanii wote nchini kuacha kuimba nyimbo zenye tungo za kisiasa ambazo lengo lake ni kuikosoa serikali ama viongozi wa nchi.

“Kama serikali ya Jamaika ingepiga marufuku wasanii wa nchini kwao wasiimbe nyimbo za siasa, basi siku kama ya leo tusingeshuhudia dunia ikiungana kuadhimisha kumbukumbu ya kifo cha kaka yetu mkuu Robert Nesta Marley…Baba Ziggy”. Alisema Afande Sele kupitia ukurasa wake wa kijamii instagram

Aidha, Afande Sele aliendelea kusema kuwa

“Heshima na umaarufu wake havikujengwa kwa tungo za mapenzi, kujisifia na blah blah nyingine bali kwa siasa ambayo ndiyo maisha yenyewe.. Nami kwa kumuenzi huyu Nabii wangu siku kama leo natamani kuropoka kwa sauti kuu kwamba ‘Ni marufuku kupiga marufuku”. Alisisitizia Afande Sele

Source: Udaku