Leo April 24 2017 millardayo.com na Ayo TV imemtafuta Msami ili kujua amelichukuliaje jambo hili na moja ya mambo aliyoyagusia ni chanzo cha ugonvi huo akisema ni baada ya AT kukuta namba ya Msami kwenye simu ya mwanamke aliyekuwa na mahusiano naye: “Ninachokijua AT alinipigia simu baada ya kukuta namba yangu kwenye simu ya mwanamke wake, lakini huyo mwanamke najuana naye siku nyingi sana na sina mahusiano naye. Akanipigia, akanambia huyu mwanamke vipi? Nikamwambia hamna, ni mshikaji wangu. Kwa hiyo naona hiyo ndio ikamtoa povu, lakini mimi I don’t care.” – Msami
Source: Millard ayo