Staa wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee amekula shavu la mwaka la kufanya kazi na Dj A-list kwasasa Marekani, Diplo.
Cash Madame ameelezea jinsi alivyopata shavu hilo,
“Waliniapproach kupitia producer wa Kimarekani ambaye ninamfahamu. Walisikia kazi zangu na ni kitu ambacho kimefanyika maybe six months ago lakini hatukikizungumzia na tulikuwa tunasubiria kazi itoke,” Vanessa aliiambia Dizzim Online. “Kwa sasa siwezi kuzungumza mengi, lakini when the work is out we will talk about it more.”
Diplo ni member wa kundi maarufu la Major Lazor, aliandaa baadhi ya nyimbo kwenye album ya Justin Bieber “Purpose” na Album ya Beyonce “Lemonade”
Source: Millard ayo