Young Dee Amchana Amber lulu

 

Soudy amewatafuta Young Dee na Amber Lulu na kupiga nao story huku ikidaiwa kuwa Amber Lulu amefuta tattoo ya taswira ya Young Dee aliyokuwa amechora.

>>>”Hamna mwanangu tu, Mnyamwezi wangu. Nimechora tattoo mpya ile ilikuwa imechoka sana ndio nikabadilisha. Sifichi, hatujazinguana chochote sisi ni washikaji siku zote. Young Dee hajawahi kuwa mpenzi wangu, ni washikaji tu. Kwani Soudy ulishawahi kumuuliza Young Dee kama mimi ni mpenzi wake? Mimi mbona nina Bwana wangu, Young Dee ni msanii mwenzangu tu.” – Amber Lulu.

Naye Young Dee alikuwa na haya alipoulizwa kuhusu kuwa mapenzini na Amber Lulu.

“Tumeachana na nani? Nimekuambia am single…sijawahi kuishi na Amber Lulu, hakuwahi kuwa mwanamke wangu. Mimi sijui maana alichora mwenyewe kwa kupenda na kama kafuta kafuta kwa kupenda mwenyewe.

“Hakuna mtu aliyemwambia, sasa itanishtua kitu gani? Mimi naona kawaida siyo breaking news labla taarifa iliyonishtua ni hii ya Msiba wa Mama Zari lakini unaniambia taarifa ya kushtua ni hiyo ya kufuta tattoo! Hebu niache nifanye kazi.” – Young Dee.

Source: Millard ayo