VIDEO: ‘Nitarudi kama Mtangazaji lakini sio kama Mwanamuziki’- Meninah

Inawezekana ulikuwa na maswali mengi kuhusu staa Meninah aliyekuwa miongoni mwa wasanii waliounda kundi la Shosteez, sasa basi March 24, 2017 staa huyo alikutana na Ayo TV & Millardayo.com kueleza sababu zilizopelekea asimame kwenye tasnia ya Bongo Fleva pia kuhusu kurejea kivingine.

‘Mwenyewe tu niliamua ili niingie kwenye masuala ya entrepreneur ndio maana nilisimama kuimba muziki kwani mshika mbili siku zote humponyoka ndio maana nikaamua kukaa zaidi kwenye biashara zangu, nimemiss kwenda studio na ukikuta muda mwingi naukosa kwasababu nautumia kukaa na familia’- Meninah

‘Mkataba wangu na Producer Lamar ulikwisha siku nyingi ila inshallah nitarudi  kwenye masuala ya media kwani sasa hivi nafanya maandalizi ya kipindi changu nitarudi kama Mtangazaji lakini sio kama Mwanamuziki’- Meninah

Source: Millard ayo