Wanasayansi kutoka Chuo Kikuu cha Hong Kong wametoa ripoti ya utafiti kuhusu uhusiano uliyopo kati ya kansa ya matiti na kula vyakula vyenye wanga nyakati za usiku ambapo mkuu wa utafiti huo Shelly Tse Lap-ah aliiambia South China Morning Post kuwa wanawake wanaokula vyakula vyenye wanga kwa wingi kuanzia saa nne usiku wako hatarini kupata kansa ya matiti.
Ripoti hiyo imeeleza kuwa kula vyakula vya wanga nyakati za usiku mnene husababisha kupungua kwa uzalishwaji wa kemikali ya Melatonin ambayo husaidia kuzuia magonjwa hatari na kuvirahisishia vijidudu vinavyosababisha kansa ya matiti kushambulia mwili kwa haraka zaidi.
Utafiti huo uliwahusisha wanawake 1,800 ambapo asilimia 1.76 waligundilika kuwa na kansa ya matiti iliyosababishwa na kula vyakula vya wanga.
“Kula vyakula vyenye wanga au Carbohydrate nyingi usiku kunasababisha: kuongezeka uzito na magonjwa kama kisukari. Mtu akipata magonjwa haya ni rahisi kupata kansa hasa kansa ya Ini, Tezi Dume na saratani ya matiti. Utafiti huu umeonesha kuwa wanawake wanaokula Tambi au Noodles wameathirika zaidi na saratani ya matiti ukilinganisha na wanawake wanaokula Mchele.” – Dr Francis Chow.
Source: Millard ayo