MWANANGU ni Biashara, Msinipangie Cha Kufanya- Skyner Ally
Skyner Ally, Udaku Spesho
Mzazi mwenzake Nay wa Mitego, Skyner Ally amewatolea povu watumiaji wa mtandao wa kijamii wa Instagram wanaomnenea mabaya mtoto wake kuwa atakuwa jike dume kutokana na mavazi anayomvalisha yatawarudia wao na kwamba yeye anaendelea kutengeneza pesa.
Skyner ameamua kutoa povu hilo baada ya watu kum-‘diss’ namna anavyomvalisha mtoto wake wa kike huku wengine wakidai mtoto ataharibikiwa na kuwa jike dume kutokana na mavazi kitu ambacho kimemfanya Skyner kuweka wazi na kudai mtoto wake anamtumia kibiashara katika kuuza nguo zake na si vinginevyo.
“Wazazi na walimu wa instagram ifike pahala mniachie mwanangu, msiniingilie wala kunipangia na hayo mnayomuombea mwanangu sijui atakuja kuwa jike dume Inshallah itawarudia nyie na vizazi vyenu ifike pahala mnielewe nipo Instagram kibiashara sipo kwa ya ajili ya show off hapana”- aliandika Skyner.
Aidha Skyner ameongeza kuwa hawezi kutumia watoto wa watu wengine katika kutangaza biashara yake wakati ana mtoto wa kufanya kazi hiyo pasipo kumlipia huku akidai mtoto wake ni wa kike japo kafanana na baba yake.
Source: Udaku