Mkubwa Fella azungumzia ukimya wa Yamoto Band

Leo March 31 2017 kupitia Leo Tena ya Clouds FM, kiongozi wa Mkubwa na Wanawe Said Fella amezungumzia minong’ono iliyozuka mitaani juu ya ukimya wa Yamoto Band ikidaiwa kuwa kundi hilo limesambaratika na kila mmoja kufanya kazi kivyake.

Mkubwa Fella amekiri Yamoto Band kuwa kimya lakini amedai kundi hilo kurudi tena upya ambapo amesisitiza kuwa bado wako pamoja ingawa kila mmoja anaishi kivyake…>>>”Maneno yalikuwa mengi juu ya Yamoto Band yetu lakini sisi tulikuwa kimya na mengi yalisemwa na leo tumeleta wimbo mpya unaitwa Basi.“

“Kila mtu alikuja pale kituoni peke yake, lakini watu wafahamu kuwa tayari Yamoto wamekuwa wakubwa kila mtu anaishi kivyake.”– Mkubwa Fella.

Source: Millard ayo