Ray C Amshauri Msanii Recho.


MWANADADA aliyerejea vizuri kwenye Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’ au Kiuno Bila Mfupa, ameibuka na kumtaka mwanamuziki mwenzake ambaye alikuwa akiimba kama yeye kwa sauti na kila kitu, Winfrida Josephate ‘Recho’ asikate tamaa bali apambane na hali yake.

Ray C anasema kuwa, ni muda mrefu hajakutana na Recho ambaye ni zao la THT na kuhusu kupotea kwake, hana cha kumsaidia zaidi ya kumshauri kwamba asikate tamaa, apambane na kufanya kazi kwa bidii ili arejee kwenye gemu kama mwanzoni alipokuwa akichipukia.
Ray C alizungumza mengi katika mahojiano hayo hivyo ungana naye hapa katika maswali na majibu ili kujua zaidi kuhusiana na maisha yake kwa sasa na muziki kwa jumla;

Akiwa kwenye pozi.
Mikito: Tunajua una harakati nyingi za kimaisha lakini baadhi ya mashabiki wako kindakindaki (die hard fans) wanatamani kujua nini Kwa sasa najisimamia mwenyewe kinaendelea kwenye muziki wako kwa sasa?

Ray C: Muziki wangu uko vizuri na nimeanza tour (ziara) yangu inayokwenda kwa jina la ngoma yangu ya Unanimaliza ambayo nitaifanya mikoani na nchi mbalimbali.

Mikito: Je, tour hiyo itakuwa kwenye nchi zipi?
Ray C: Nimeanza na Tanga halafu nitaenda Oman na Rwanda, halafu na nchi nyingine nyingi ambazo nitatoa ratiba hivi karibuni.
Mikito: Je, kwenye hiyo tour utakuwa na nani?

Ray C: Nina timu yangu ndiyo nitakwenda nayo.
Mikito: Nini siri ya mafanikio yako kimuziki kwa sasa?

Ray C: Siri ni bidii yangu tu katika kazi, hakuna kingine. Mikito: Je, una meneja?
Ray C: Hapana, sina, najisimamia tu mwenyewe.

Mikito: Vipi hiyo tour ulitafutiwa na nani?

Ray C: Wimbo wangu wa Unanimaliza umekubalika sana masikioni mwa watu ndiyo iliyonifungulia milango ya kazi.

Mikito: Kuna baadhi ya wasanii wenzako waliachana na matumizi ya madawa ya kulevya, lakini hivi karibuni wamegundulika kwamba wanaendelea kutumia akiwemo Chid Benz, unawaambiaje au unawasaidiaje kwa sababu wewe umeweza kuachana kabisa na matumizi hayo ya madawa?
Ray C: Hilo halinihusu kabisa.

Mikito: Kwa upande wa maisha yako binafsi, una mchumba au mpenzi?

Ray C: Sina wala sitaki. Mikito: Kwa nini na unaishije mrembo uliyekamilika kama wewe?
Ray C: Sina muda wa mambo hayo kwa sasa, niko busy na kazi.

Mikito: Nini ushauri wako kwa wasanii wa muziki hasa wa kike?

Ray C: Ninawashauri wafanye kazi nzuri, waachane na kiki za mjini kwa sababu hazina mpango wala hazidumu.

Mikito: Kwa upande wa Watanzania unawaambia nini kuhusiana na muziki wako na maisha yako kwa sasa?

Ray C: Wapambane tu na hali zao.

Source: Udaku.

Facebook Notice for EU! You need to login to view and post FB Comments!