Duniani Imegunduliwa sidiria yenye uwezo wa kutambua kansa kwa wanawake

Mwanafunzi kutoka Chuo Kikuu Mexico ameshika headlines duniani baada ya kutengeneza sidiria ‘Brazia’ ambayo ina uwezo wa kugundua saratani ya matiti katika hatua za mwanzo,Teknolojia hii ya kugundua saratani kwa haraka na ufanisi imetajwa kuwa ya kwanza kuwahi kutengenezwa na mtu yoyote duniani.

Julian Rios Cantu, 18, ametajwa kuwa mjasiriamali mgunduzi mdogo zaidi duniani kuwahi kutengeza sidiria ambayo imewekwa kifaa maalum ambacho kina uwezo wa kupima hali ya joto na mtiririko wa damu katika matiti, hivyo kuweza kuonesha dalili za ugonjwa wa saratani ya matiti.

Akizungumza na BBC Julian Rios Cantu amesema kuwa alisukumwa kutengeneza siridia hizo ili kuwa msaada kwa wanawake wote duniani baada ya mama yake kugundulika na ugonjwa wa saratani ya matiti. Sidiria hizi zimetabiriwa kupunguza athari zinazoletwa na ugonjwa wa saratani ya matiti kwa asilimia 70

Source: Millard ayo