Kawaida ya simu zote za Smartphones zimekuwa zikiongezeka size toka kizazi kimoja hadi kingine tukishuhudia matoleo kadhaa ya simu hizo katika size tofauti tofauti, lakini sasa imekuwa tofauti baada ya kampuni moja kuamua kuja kivingine.
Kampuni ya Unihertz imeamua kutengeneza smartphone iliyopewa jina la Jelly ambayo itakuwa smartphone ya kwanza ndogo zaidi duniani ikiwa na uwezo wa kuunganisha 4G wakati ikiendelea kutoa huduma kama ambavyo inatoa smartphones nyingine ghali.
Jelly itakuwa na sifa na uwezo kama ambao unapatikana katika smartphones nyingine na zitaingia sokoni August mwaka huu kwa matoleo mawili ya standard na pro.
Source: Millard ayo