Tanzania hakuna mashabiki wa kweli

 

Msanii wa muziki wa hip hop Bongo, One the Incredible amesema wasanii bado hawana mashabiki na ndio sababu ya kutokuwepo kwa mauzo ya albamu. Rapper huyo ambaye ameachia ngoma mpya ‘Danga’, ameeleza licha ya changamoto hiyo bado amekuwa akitoa albamu kwani ana baadhi ya mashabiki ambao wamekuwa wakinunua kazi

“Huwa natoa albamu, mimi sio msanii wa single, sijui kuhusu watu wengine lakini kitu kimoja ninachokifahamu kuhusu industry ya Tanzania ni kwamba wasanii kwa asilimia kubwa bado hawana mashabiki. Kuna watu wanapenda muziki, kuna watu wanadownload, kuna wanashare lakini sio mpenzi wa sanaa tunaweza tukaandaa show tukahusisha wasanii wengi wakajaa watu 30,000 lakini masanii mmoja akaandaa show yake hawafiki watu hata 1,000, kwa hiyo inaonyesha mashabiki hamna au industry haijajengwa kuwaelewesha wafuatiliaji wa muziki jinsi ya kuwa mashabiki. “Kwa upande wangu nimekuwa na fan base yangu in way imekuwa inakua, haijafika pale ambapo nataka iwepo lakini na fan base nzuri tu ambayo inatokana na mimi kufanya albamu,” amesisitiza One

Source: Teamtz