Lulu amuandikia Dr. Cheni Waraka mzito

Mwigizaji staa wa Tanzania Elizabeth Michael maarufu Lulu leo July 19 ametumia Instagram yake kumuandikia salamu za upendo na shukrani Mwigizaji wa siku nyingi Dr.Cheni ambae leo ni kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa.

Lulu aliandika “Happy Birthday Baba…! Asante Kwa Kuwa Baba Mlezi Kwa Miaka Yote Tangu Uliponijua…..Asante Kwa Kuwa Mtu Wa Kwanza Uliyekiona Na Kukiamini Kipaji Changu Na Kuhakikisha Hakiishii Kwenye Macho yako Tu….Ninaweza Kusema Mpaka Hapa Nilipofika Kuna Mchango Wako Mkubwa sana…Mbali Na Wakati Wa Furaha Hujawahi Kuniacha Wala Kunikana Katika Shida Na Hata Aibu Zangu…..Sidhani Kama Kuna Kitu Naweza Kukulipa Wewe na Familia Yako Zaidi ya Kumuomba Mungu Aendelee Kuwatunza❤️Unapoongeza Mwaka Mwingine Mungu wangu Ninayemuamini Akakuongeze Katika Kila Eneo…..Afya,Uzima,Maarifa,Uchumi na Akakutane Na Haja Zoooote Za Moyo Wako. @drchenitz @drchenitz @drchenitz”

Source: Millard ayo