Wayne Rooney Ahukumiwa.

Nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya England anayeichezea Everton kwa sasa aliyojiunga nayo msimu huu akitokea Man United Wayne Rooney, amekutwa na hatia ya kuendesha gari akiwa amelewa ikiwa ni kinyume na sheria.

Rooney baada ya kufikishwa Mahakamani alikiri kosa na mahakama kuamua kumfungia miaka miwili kuendesha gari, pamoja na kufanya kazi za kijamii bila malipo kwa saa 100 na kulipa pound 170 baada ya kufika Mahakamani.

Kwa kawaida nchi za England na Wales mtu anaruhusiwa kuendesha gari akiwa amekunywa pombe kwa kiwango cha microgrammes 35 lakini Rooney alipimwa na kukuta amekunywa microgrammes 104, baada ya hapo Rooney ameamua kuomba radhi kwa jamii, familia yake na kila mmoja anayemsapoti.

Statement ya Rooney ya kuomba radhi kwa kilichotokea

Kama utakuwa unakumbuka vizuri Wayne Rooney alikamatwa na Polisi September 1 2017 Wilmslow, Cheshire na baadae kuachiwa kwa dhamana baada ya kukutwa anaendesha gari akiwa amelewa, kitu ambacho ni kinyume na sheria za England.

Source: Millard ayo.

Generic selectors
Exact matches only
Search in title
Search in content
Post Type Selectors