Birdman Yuko Njiani Kuja Tanzania.

Rapper na Producer maarufu wa Marekani Bryan Williams a.k.a Birdman ambae Wasanii wengi wamepitia kwenye mikono yake akiwemo Lil Wayne, Nicki Minaj na Drake, ametangaza rasmi kuja Tanzania.

Birdman ametoa tano za nguvu kwa upendo ambao nchi hizi za Afrika zimeuonyesha kwake Nigeria, Kenya, Tanzania, Gambia na Ghana na baada ya kuzipa tano za nguvu akaandika atazitembelea nchi hizi February 2018.

Iwapo Birdman atakuja Tanzania, atakua ameingia kwenye orodha kubwa ya Waamerika weusi mastaa waliowahi kuitembelea nchi hii akiwemo Mtangazaji Oprah na Mwimbaji Usher Raymond.

Source: Millard Ayo.