Rodriguez alichowafanya mabeki wawili

James Rodriguez alifunga bao moja na kusaidia ufungaji wa mengine mawili alipoanza mechi yake ya kwanza Bundesliga katika klabu yake mpya ya Bayern Munich.

Aliwasaidia kulaza FC Schalke 04 3-0.

Rodriguez, ambaye yuko Bayern kwa mkono kutoka Real Madrid ya Uhispania, alifungia Bayern bao lao la pili mechi hiyo.

Katika bao la kwanza, beki Naldo alinawa krosi ya mchezaji huyo wa Colombia na kuwazawadi Bayern mkwaju wa penalti ambao ulifungwa na iRobert Lewandowski.

Rodriguez aliwachenga mabeki wawili kabla ya kuupaisha mpira juu ya safu ya ulinzi ya Schalke na Arturo Vidal akafunga.

story@moodyhamza