Azidishiwa Fedha kwenye Account Yake.

Utafanya nini pale utakapotembelea akaunti yako ukakuta kuna nyongeza ya Dollar Milioni 4.6 ambazo hazikutakiwa kuwemo humo? Imetokea kwa msichana mmoja ambaye ushawishi ulimzidi.

Unaambiwa baada ya Bank kuingiza kiasi cha Dollar Milioni 4.6 zaidi ya Tsh. Bilioni 10 kwenye akaunti yake kwa bahati mbaya, hakutaka kupoteza muda wala kutoa taarifa za kutokea makosa hayo, badala yake akaanza kuzitumia hata kabla ya mtu yeyote kujua.

 

Msichana huyo anafahamika kwa jina la Christine Jiaxin Lee, ambaye ni Engineer kutoka Malaysia mwenye umri wa miaka 21, alikutana na bahati hiyo wakati anasoma Australia.

Makosa yalifanywa na Bank na kuingiza katika akaunti yake kiasi cha Dollar Milioni 4.6 ambapo alishindwa kuzuia ushawishi na akaanza kufanya shopping na alipokuja kubainika alikuwa amebakiwa na Dollar Milioni 3.3.

Lakini ajabu ni kwamba alitumia fedha nyingi katika kununua mikoba.

Source: Millard ayo