RAIS Zuma Kutua Nchini Tanzania Leo

Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma anatarajiwa kuwasili nchini leo (Jumatano) saa 10.00 jioni. Rasi Zuma atakuwa nchini kwa ziara ya siku tatu kufuatia mwaliko kutoka kwa Rais John Magufuli. Ziara hiyo inalenga kuimarisha uhusiano wa kibiashara kati ya Tanzania na Afrika Kusini. Katika ziara hiyo Rais Zuma ataandamana na mawaziri sita pamoja na wafanyibiashara zaidi ya 80 kutoka Afrika Kusini. Pia atashirikia mkutano wa wafanyabiashara, atazindua jengo Ubalozi wa Afrika Kusini na kutembelea Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete.