Baada ya ‘WAPE’ Bongolos wanakuja na hii kutoka Bongo Records

Jina la P Funk siyo ngeni katika masikio ya wengi ambao wamekuwa wakifuatilia Bongofleva kwa miaka mingi sana. Ni mmoja wa Maproducer waliofanikiwa kwa kiwango kikubwa kuukuza muziki wa Tanzania kwa kuusimamia na kuutegeneza.

Good news kutoka kwa star producer huyo ni kwamba mbali ya kutengeneza beats pia amejikita kusimamia na kuongoza kundi la muziki linalojulikana kama Bongolos ambalo tayari linatamba na hit single yao ‘Wape’.

Ayo TV na millardayo.com zimepiga story na Bongolos linaloundwa na Drew na Tamu ambao wamefunguka namna walivyokutana na P Funk na kufanya naye kazi huku wakielezea pia mipango yao ya baadaye.

Source: Millard ayo