Mr T Touch amsaini Young Dee kwenye label yake, Touchez Sound Records


Young Dee amesaini mkataba wa miaka mitatu na label ya Producer Maarufu Mr T Touchez, Touchez Sound Records.

“Mimi nimeingia mkataba mrefu wa miaka mitatu na Young Dee. Ataendelea kuwepo chini ya Touchez Sound na mimi ndiye nitakayesimamia na kutengeneza beat za nyimbo zake zote. Nia yangu ni kumfanya afanye vitu tofauti na alivyokuwa akifanya hapo awali kwa kuwa mimi namuona ni msanii mwenye biashara,” Mtayarishaji huyo wa muziki amekiambia kipindi cha E-News cha EATV Ijumaa hii.

Young Dee alikuwa anasimamiwa kazi zake na MDB ya Max Rioba kabla ya kutangaza kuachana naye mapema mwanzoni mwa mwaka huu.

Source: Teentz