Mashabiki walia na penzi la Jux.

Staa wa muziki wa kizazi kipya kutoka Tanzania, Juma Jux na muimbaji Vanessa Mdee kwa mashabiki imeonekana kuwa walipendezwa sana na uliokuwa uunganiko wao kama wapenzi na huku maoni ya wengi yakionekana kuwaomba warudiane na baadhi yao kujaribu kutuma maombi kwao.

Maoni ya wengi yameibuka wakiwataka wamalize tofauti yao na warudi kuwa wapenzi kama zamani kulingana na kile walichokisikia kutoka kwa Jux ambapo amebainisha kuwa wazo la wimbo wake mpya lilizaliwa kutokana yeye kuwa kayika panda shuka za kimahaba na Vanessa.

Hata hiivyo kwa maoni ya baadhi ya waliomsikia Jux katika maojiano imehisiwa kwamba waligundua kuwa bado kuna mahaba ya dhati kwa Jux, hivyo sio vyema kama hawatarudiana.

Source: Dizzim Online.