Diamond Platnumz Atoa Shavu Kwa Nyashiski

Mkongwe wa muziki na mkali wa ngoma ya ‘Mungu Pekee’ Nyashinski kutoka nchini Kenya amepata ushirikiano kutoka kwa Staa wa Bongo Fleva Diamond Platnumz kusambaza taarifa kwa mashabiki wake na wanaopenda muziki wa Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla ili aweze kupata ushindi wa tuzo ya MTV EMA kupitia kipengele cha Best African Act.

Kipengele hicho cha BEST AFRICAN ACT kunawaniwa na wakali wanaofanya vizuri Barani Afrika ambao ni pamoja na Babes Wodumo anayeiwakilisha Afrika Kusini, C4 Pedro kutoka Angola, DaVido kutoka Nigeria, Nasty C kutoka Afrika Kusini na WizKid kutoka Nigeria.

Nyashinski katika kuupokea ushirikiano wa Diamond Platnumz imeonesha wazi kuwa nikitu kikubwa kwake na kuheshimu hatua hiyo ya ushirikiano ambayo imeonesha wazi kuwa kuna suhirikiano wa wasanii wa muziki wa Tanzania na nchi ya Kenya.

Source: Dizzim Online.