Ratiba ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya droo, Yanga vs ?? TP Mazembe vs ??

Baada ya Dar es Salaam Young Africans kutolewa katika michuano ya Club Bingwa Afrika na Zanaco FC ya Zambia na kuangukia Kombe la shirikisho barani Africa, leo March 21 2017 shirikisho la soka barani Afrika CAF limechezesha droo ya mtoano wa mwisho.

Mwaka huu ambapo mashindano ya CAF yamefanyiwa mabadiliko ya Club Bingwa na Shirikisho na kuweka Makundi manne tofauti na misimu iliyopita makundi mawili, imechezesha droo na Yanga kuangukia dhidi ya MC Alger ya Algeria, Yanga itaanzia nyumbani na baadae kurudiana Algeria.

Timu zilizoanza kuandikwa zote zitaanza kucheza nyumbani mchezo wake wa kwanza

Source:Millard Ayo