Mwanamuziki A.Y Ampongeza Mpenzi Wake.


Baada ya kumvisha pete uchumba wake wiki iliyopita, rapper A.Y amempongeza mpenzi wake huyo kwa kuhitimu masomo yake.

Kupitia mtandao wa Instagram, rapper huyo amemposti na kumpongeza mrembo huyo kwa kuandika “I’m so proud of you..Congratulations Engineer Remy

Kwa mujibu wa vyanzo vya karibu vimedai kuwa huwenda rapper huyo hivi karibuni akauaga ukapera rasmi kwa kufuata nyayo za mswahiba wake Mwana F.A

Wiki chache zilizopita msanii huyo aliudhulia harusi ya msanii mkongwe na Mbunge wa Mikumi Joseph Haule a.k.a Proffesa Jay ambaye alifunga ndoa jiji Dar es salaam na kuudhuliwa na mastaa kadha akiwemo Diamond Platnum,Harmonize, Lady Jay Dee, Elizabeth Michael na wengineo.

                                              Source: Udaku