”Kitu muhimu ni mechi mbili, alama sita na nafasi nzuri katika kombe la vilabu bingwa”

Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho amesema kuwa kikosi chake kinakaribia kufuzu katika mechi za muondoani baada ya kuilaza CSKA Moscow nchini Urusi.

Romelu Lukaku alifunga mabao mawili, huku Anthony Martial akifunga penalti na Henrikh Mkhitaryan kufunga bao la nne na kuifanya Unitedkundeleza rekodi yao ya kutofungwa kwa asailimia 100 katika kundi A.

Kikosi hicho cha Old Trafford kilikuwa kimeshinda mechi moja pekee kati ya 10 za ugenini katika kinyanganyiro hicho, lakini mabao mawili katika dakika za kwanza 18 ziliifanya United kupata ushindi wa rahisi.

”Kitu muhimu ni mechi mbili, alama sita na nafasi nzuri katika kombe la vilabu bingwa”, alisema Mourinho ambaye kikosi chake kiliishinda Basel 3-0 katika mechi ya funguzi.Tumesalia na mechi nne kucheza lakini tulianza vyema na tunakaribia”.

story@moodyhamza