mambo matano tuliyojifunza katika michezo ya Ligi Kuu Bara

Goal inakuletea mambo matano tuliyojifunza katika michezo ya Ligi Kuu Bara iliyochezwa siku ya Jumamosi na Jumapili

Bado klabu za Simba, Mtibwa  Sugar na Yanga zimeendelea kukabana koo kileleni kwa alama zao 15 kwa kila mmoja huku Azam, Singida United nao wakiwa hawako mbali, huku hali bado ni tete kwa klabu za Majimaji, Stand United na Kagera Sugar baada ya kupoteza michezo yao

Goal inakuletea mambo matano tuliyojifunza katika michezo ya Ligi Kuu Bara iliyochezwa siku ya Jumamosi na Jumapili

1. Imani za kishirikina bado changamoto kwenye Ligi yetu

Bado imani za kishirikina zimeendelea kutawala sana kwenye mpira wetu, katika mechi ya Simba na Njombe Mji kulitokea sintofahamu kwenye lango la kuingilia ndani baada ya mashabiki wa Simba kuwashutumu wale wa Njombe Mji kuwa kuna vitu wanataka kuvifanya mlangoni hivyo kupelekea kuvutana kwa pande hizo mbili

@moodyhamza