Msanii kutoka label ya WCB Wasafi, Harmonize amesema ameamua kurudi shule ili kujifunza kiingereza.
“Niko najifunza,” Harmonize alifunguka kwenye kipindi cha XXL cha Clouds Fm “Unajua watu wanashindwa kuelewa kitu kimoja, kila kitu ni hatua, hasa kwa sisi ambao tulikosa elimu bora. Sasa hutakiwi ku-concentrate sana na comments za instagram kwasababu kila mtu anakuwa na ubongo wake na akili yake, kuna mtu kaamka vibaya kakosa kazi ya kufanya na kuamua kuingia kwenye account na kutukana the way anajiskia. Ukisema uconcentrate na watu wanao comment vibaya mwisho wa siku utaanza kuwajibu watu.” Alisema Harmonize
.