Mimi Mars ataja sifa za mwanaume anayemtaka

Msanii wa kike anaechipukia kwenye game Marianne Mdee maarufu kama  ‘Mimi Mars’ ambaye ni mdogo wake na Vanessa Mdee amefunguka na kutaja sifa za mwanaume ambaye anahitaji kuwa naye kwenye mahusiano au kuwa mume wake kabisa.

“Mimi siwezi kutoka na mtu maarufu na namuomba Mungu hilo jambo apishie mbali kabisa,” Mimi Mars alifunguka kwenye kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio. “Kwani mimi napenda nikiwa na mwanaume au mume nikirudi nyumbani nimkute, awe mpole mpole ila asiwe kwenye mambo haya ya muziki, awe mfanyakazi tu ambaye labda anatoka nyumbani asubuhi na kurudi nyumbani mapema ila asiwe mtu maarufu”.

Mbali na hilo msanii huyo amesema kuwa mwezi wa nne anaweza kuachia wimbo wake mwingine baada ya kupokelewa vyema na ngoma yake ya ‘Sugar’ kwani anadai mashabiki wamekuwa wakimshauri kuwa asikawie kutoa wimbo mwingine.

SOURCE BY: TEENTZ