One The Incredible atoa ushauri kwa serikali ya Magufuli


Msanii wa muziki wa kizazi kipya cha rap Tanzania One The Incredible ametoa mgawanyo wa majukumu unaoweza kusaidia katika ulimwengu wa sanaa ili wasanii na wahusika wote wa sanaa waweze kufaidika na kazi ya sanaa yao.

Akizungumza na Dizzim Online One The Incredible amesema kuwa mpaka sasa kumekuwa na msukumo mdogo wa kila mhusika wa sanaa kuhakiksha anafanya jambo stahiki akiitaja serikali kuwa chombo kikuu cha kwanza kufanya chini juu kusimamiza na misingi itakayo faidisha kila mdau wa wasanii wahusika.

“Mimi naamini chochote ambacho kinaweza kufanyika katika ulimwengu wasanaa kinahusika na wasanii wenyewe, Serikali inachoweza kufanya ni kusimamia vile ambavyo tu sheria inasimamia haki za wasanii. Nadhani serikali yetu inahitaji kujenga mazingira bora zaidi kwenye suala la jinsi sheria inavyo apply kwenye sanaa, msanii na jamii husika ya wasanii na sanaa yao” Alisema One.

Hata hivyo one ameongeza kusema kuwa kama kila upande utafanya kazi kwa nafasi yake muziki utakuwa na nafasi ya juu kufikia malengo ya kila msanii na wasanii wahakikishe wanafanya kazi zenye hadhi kwakuwa serikali haiwezi kumuandalia au kumtungia wimbo mzuri.

Source: Dizzimonline