Ugomvi Wa Diamond Na Alikiba Washindikana.


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amesema mvutano wa Diamond na Alikiba hauna haja ya kuhusuluhisha ikiwa ni wa kiuweledi na kitaaluma.

Dkt. Mwakyembe amesema haamini kama tatizo ni kubwa kiivyo bali ni kitu chenye afya tu kwa sababu kinaleta ushindani mzuri ambao unapeleka muziki katika ngazi nyingine.

“Kama kuna ushindani kati ya Alikiba na Diamond ambao ni kiuweledi, kitaaluma basi mimi nafikirii tungeuendeleza zaidi, hamna sababu ya kuwasuluhisha, waendelee kushindani vizuri tupate miziki mizito.

“Kwa hiyo mimi naomba Watanzania wachukulie mvutano huo ni mzuri katika tasnia, mradi mimi sijasikia watu wameshikiana mapanga,” ameongeza.

Katika hatua nyingine Dkt. Mwakyembe ameendelea kusisitiza dhamira yake ya kuwaita pamoja Diamond na Alikiba ili kufanya ngoma pamoja kama alivyowahi kuhaidi hapo awali.

“Ukifika muda nitawaita wote watanisikiliza tu watatunga wimbo mmoja wa kukata na shoka pengine bara nzima la Afrika litatikisika, ni vijana wenye vipaji lazima tuendelee kuwatia moyo,” amesema.

Source: Udaku.