‘Kujua Kuongea kiingereza ni vizuri lakini sio Ujanja.

Hii inaweza kuwa salaam kwa wote ambao mara nyingi hamjiamini na mazungumzo yenu hasa yanapofikia hatua ya kubadili lugha na kutumia kiingereza,miezi michache iliyopita Alikiba alikua na mahojiano na baadhi ya Radio nchini South Africa mahojiano ambayo yalikua yakifanyika kwa lugha ya Kiingereza.

Kwenye comment nyingi watu wengi walionekana kama kumponda kuwa hajui kuzungumza vizuri lugha hiyo,sasa leo ameamua kuliweka wazi>>’Kuongea kiingereza ni vizuri lakini sio ujanja kutokujua kiingereza fresh kabisa na vile vile sio ujinga sio ujinga kabisa kuna wengine wanafanya kazi na maisha yao yanaenda’

‘Mimi lugha yangu kiswahili wewe unajua mimi nimesomaje?Napokua nimekosea ni ubinadamu binadamu si tunakosea lakini namshuruku Mwenyezi Mungu naweza kuongea kiingereza mimi na ukanielewa lakini sisemi mimi kama najua kiingereza,wenyewe wazungu ukiwauliza unajua kiingereza wanakwambia tunajua kidogo’

‘Sina juhudi yoyote ya kuendelea kujinoa na sijajifunza sehemu yoyote kiujanja ujanja hivi hivi kwa sababu naongeleshwa kiingereza na najibu,kwanini niwe na juhudi za kujifunza wakati hainiingizii chochote,Mi naimba kiswahili na naingiza mpunga na maisha yangu yanaenda vizuri na naongea kiswahili’ – Alikiba.

Source: Dizzimonline