Aunty Ezekiel ataja idadi ya watoto anaotaka kumzalia Mose Iyobo

                      

Msanii wa Filamu nchini Aunty Ezekiel ameweka wazi ni watoto wangapi ambao angependa kuzaa na Dancer wa Diamond Platnumz ‘Mose Iyobo’ ambae hata hivyo tayari amemzalia mtoto mmoja.

Kupitia kipindi cha Kikaangoni cha EATV Aunty Ezekiel amesema anatamani kumzalia Mose Iyobo watoto watatu tu,inatosha sana kwani amezingatia vigezo vya kiuchumi.

“Mimi ni mkubwa kwa Mose, ninamzidi umri lakini akili zake ni zaidi ya umri wake. Ningependa nimzalie watoto watatu“Amesema Aunty Ezekiel.

Akizungumzia jinsi walivyokutana Aunty amesema hakuamini kama angekutana nae kwenye ndege na kuwa mmewe kwani walikuwa safarini kuelekea Afrika Kusini na walipigana Kiss tu na ndiyo hapo mapenzi yakaanza.

                                  Source: Udaku