kupitia Leo Tena ya Clouds FM Geah Habibu ametuletea HekaHeka ambayo imetokea Kigogo jijini Dar es Salaam ambapo dada mmoja anadaiwa kujifungia chumbani na mtoto wa jirani yake mwenye umri wa miaka mitatu.
Inadaiwa kuwa dada huyo hakuwa na mazoea na mtoto huyo lakini kilichoshangaza kitendo chake cha kumchukua mtoto huyo na kujifungia naye chumbani ambako licha ya kubanwa hajasema kwa nini alifanya hivyo ingawa mtoto huyo alikuwa analia.
Source: Millard ayo