Boitumelo “Tumi” Molekane ni moja ya rappers wa Afrika Kusini wanaoheshimika zaidi kwa uandishi wao. Lakini kitu ambacho wengi hawakifahamu kuhusu Tumi, ni kuwa alizaliwa nchini Tanzania, August 16, 1981.
Wazazi wake walikimbia machafuko nchini Afrika Kusini kuja kutafuta hifadhi nchini enzi za ubaguzi wa rangi. Aliishi Tanzania hadi akafikisha umri wa miaka 12 na ndipo wazazi wake waliporejea tena nchini mwao, mwaka 1992 na kuishi Soweto.
Tumi anasifika kwa hip hop yake inayozungumzia masuala ya kijamii na hivyo kujitengenisha na rappers wengine wa nchini humo. Pia ana label yake mwenyewe, Motif Records.
Source: Dizzim online