Rapper wa Afrika Kusini, Nasty C ameingia studio na mshindi wa BET, Viewers Choice Best International Act, RayVanny.
Mmoja wa waandaji wa Show iliyomleta rapper huyo anayekimbiza kwasasa Afrika ‘Noir’ ametweet picha ya Nasty C akiwa studio za WCB akirekodi ngoma mpya na Ray Vanny.
Nasty C ambaye alikuja Tanzania kwa ajili ya show, alipofika alisema Tanzania anawafahamu Diamond, Ray Vanny na Nandy na angependa zaidi kufanya kazi na Ray Vanny.
Source: Team Tz