CHEGE AONGEA KUHUSU DIAMOND

Ni wiki 4 tu ndio zimepita tangu idondoshwe hitsong ya “WaacheWaoane”yakwake Chege ambayo kamshirikisha Diamond Platnumz.Ngoma ambayo mpaka sasa imeonekana kuvunja rekodi katika ngoma zote ambazo amewahi kufanya msanii Chege kwa kupata mafanikio makubwa sana tena ndani ya muda mfupi tu, ukilinganisha na ngoma zilizopita.
Chege ameshindwa kuzificha hisia zake za shukrani na kuamua kuuambia umma kwamba uwepo waDiamond Platnumz katika ngoma ile ni chachu kubwa ya mafanikio ya ngoma hiyo.
Chege ameiambia Perfect255 kwamba “Kila video ina nguvu yake, Sweety Sweety ilipokelewa vizuri na ina viewers wengi lakini “Waache Waoane” imekuwa ni zaidi tena kwa muda mfupi sana na yote nafikiri ni kwasababu nimefanya collabo na mtu wa nyumbani ambaye anapendwa sana na pia ana team kubwa ambayo inajua kusapoti na ninafikiri ni hicho ndio kimesababisha ngoma hiyo kufanya vizuri.”@joplus_
Sio hayo tu, ni mengi ambayo ameyazungumza Chege na interview nzima hii hapa chini unaweza kuitazama.


Source: Raha za walimwengu