WEMA Sepetu Akosa Ladha yake ya Zamani Mwenyewe Adai Siasa Imemfanya Asing’ae

Kwa mujibu wa Wema Sepetu, zamani alikuwa anabipu lakini baada ya kubadili upepo na kuhama Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuhamia Chama cha Demokrasia na Maendele (Chadema) amejikuta ‘akifi chwa’ na kushindwa kuwika hivyo kuhisiwa kuwa ufalme wake unataka kupotea kutokana na staili ya maisha ya upande huo ambayo hayataki mbwembwe nyingi.

Nyendo za Wema tangu siku ya kwanza alipotangaza mabadiliko yake ya maisha ya kisiasa na kuhamia rasmi Chadema ambapo limebaini kuwa kwa kiasi fulani baadhi ya ndugu na mashabiki wake wamekosa ladha yake ile ya zamani.

Wamekosa ile ladha yake ya kujichanganya kila kona na kusababisha matukio yaliyokuwa yakimfanya kutokaukiwa na vituko na vijimambo, jambo ambalo kwa sasa ni nadra sana kujitokeza.

Akizungumzia na Ijumaa juu ya kufi chwa kwake, Wema anasema kwamba, siku zote unapoamua kuanza maisha mengine lazima ukubali kubadilika kwa kila jambo hivyo kwa kipindi hiki ambacho ameamua kuanza maisha mapya ya siasa, ili aweze kufi kia malengo na dhamira yake, hana budi kuchagua namna nyingine ya maisha japokuwa kuna wale ambao hawatakubaliana naye wala kuridhika na maisha aliyoyachagua kwani wapo ambapo staili yake hiyo itawagharimu.

Wema anasema kuwa, anajitahidi kuendelea kumfanya mtu ampendaye asione mabadiliko ya maisha yake, lakini pia lazima kila mmoja atambue kuwa siku na umri havisubiri. Hivyo ni lazima aanze mapema kuchagua vitu vya msingi vya kujihusisha navyo.

Wema anasema:

“Kweli kuna watu wengi wanasema nimepotea japo sijajua wa

namaaninisha nimepotea wapi, maana nilichoamua kukifanya kwa sasa ni kuangalia mambo ya muhimu na hasa kwenye siasa ambayo ndiyo sehemu niliyoichagua kuwekeza asilimia kubwa ya maisha yangu.

Source: Udaku