Diamond Platnumz Ataja Jina La Album Yake Mpya

Diamond Platnumz amelitaja jina la album yake mpya. Akizungumza kwenye kipindi cha The Trend cha NTV Kenya Ijumaa hii, staa huyo wa Marry You, amesema album yake itaitwa, Nothing But Bongo Flava.

Mapema mwezi huu kwenye mahojiano na Dizzim Online alieleza kwanini ameamua kuja na album ya Bongo Flava tu.

“Kwanini natoa album yangu ya Bongo Flava? Ni kuonesha kwamba ‘Diamond mnayemsema ninyi ni huyu, ila Diamond huyu anatafuta soko lake na riziki nyingine.’ So ilikuwa tabu kwakuwa kuna muziki mwingine unajua kabisa huu ni wa uongo, lakini huo muziki ndio utakaokufanya uvuke.”

Source: Dizzimonline