Feza kayaweka wazi mahusiano yake kwa Rayvanny

Mrembo kutoka Bongoflevani na Mtangazaji wa radio Choice FM Feza Kessy amepita kwenye studio za Millard Ayo na moja kati ya maswali aliyoulizwa kwenye On Air With Millard Ayo ni kuhusu  mahusiano yake na mastaa wawili kutoka Bongoflevani, Rayvanny na Quicky Rocka.

Unajua mimi nikiamua kutoka na mtu wala sitajificha nitaweka wazi tu na kuhusu ukaribu wangu na Rayvanny ni kwa ajili ya kazi na ni rafiki yangu‘>>> Feza Kessy

Kumekuwa na maswali mengi kuhusu Quicky Rocka na hii ni kwa sababu nilionekana naye kwenye red capet kwenye usiku wa Love Melodies and LightQuicky ni rafiki yangu pia alafu ule usiku yeye alikuwa na mpenzi wake ambaye mimi ni rafiki yangu lakini watu hawakumuonaFeza Kessy

Source: Millard ayo