Alichokisema Jacqueline Wolper kuhusu kuendelea kufanya kazi na WCB

May 15, 2017 Kupitia U-heard Muigizaji staa wa Bongo Movie Jacqueline Wolper ambaye alikuwa mapenzini na mwimbaji star Harmonize  kutoka WCB amefunguka juu ya kuendelea kufanya kazi na WCB licha ya kuachana na aliyekuwa mpenzi wake Harmonize.

Soudy Brown alipiga story na Wolper kutaka kujua ukweli wa madai hayo: “Mnajua, Wasafi nilijuana nao kabla yake. Kwa hiyo, ni kama ndugu zangu sasa hivi. Siwezi kuwa nao mbali, nikiwa na issue yangu, wanafanya na wakiwa na issue yao nitafanya.

“Soudy, ulishasikia namuongelea huyu mtu kwa lolote? Yeye ameshaongea, mimi siwezi kumuongelea mtu ambaye hayupo kwenye maisha yangu wala hatokuwa kwenye maisha yangu. Sitaki kumuongelea huyo mtu kabisa.” – Jacqueline Wolper.

Source: Millard ayo