Ushawishi wa mke wa star ulivyomtoa Alikiba kwenye Soka hadi kuimba

Alikiba ni miongoni mwa waimbaji wanaofanya vizuri katika industry ya muziki Tanzania na Bara la Afrika kwa ujumla ambapo amepata mafanikio na kujikusanyia mashabiki wengi, lakini kabla ya kufikia hatua hiyo mwimbaji huyo aling’ara sana kwenye soka kabla ya kushawishiwa kuingia kwenye muziki.

Staa mkongwe kutoka Bongoflevani Abby Skillz amesema kuwa mke wake Maria ndiye alimshawishi amwachishe Alikiba kucheza mpira na ampeleke kwenye muziki kwa sababu alikuwa na sifa ya kuwa mwanamuziki mzuri tofauti na soka.

Abby Skillz amesema kupitia 255 ya XXL kuwa alifuatwa na Alikiba na kumwambia kuwa anaweza kucheza mpira hivyo aliamua kumpa nafasi kwenye mpira, lakini alipoanza kuimba mke wake Maria akamshawishi amchukue ili afanye naye kazi.

“Alikiba alikuwa mchezaji mpira ambaye alikuwa anakuja pale kwenye timu yetu iliyokuwa inaitwa Mwiba F.C maeneo ya Kariakoo. Nilipomjaribu akawa anacheza vizuri. Alikuwa anafunga mabao mengi. Nilipomsikiliza kwenye kuimba pia alikuwa ananiimbia nyimbo zangu. Alikuwa anaimba vizuri mpaka anapitiliza.

“Mama watoto wangu, Maria ndiye aliyenishawishi, akiniambia kuwa Alikiba anajua kuimba. Kweli nikawa niko naye popote. Tukaanza kwenda naye na mpaka nikawa namshirikisha. Alikuwa anaimba vizuri sana hata nikavutiwa. Nikampenda na akawa kama familia yangu, kama ndugu yangu. Ndio maana na yeye mpaka leo ananishikilia maana na mimi nilimshikilia vizuri.

“Alikiba amewazidi wengi kwenye uimbaji kwa sababu alikuwa ana melody kali, mtunzi na ana sauti. Nilipokuwa namchukuwa na kumwambia aimbe kwenye kundi la watu, walikuwa wanamtunza kabla hajawa staa.” – Abby Skillz.

                                                           Source: Millard ayo