Mwanamziki wa kike wa Bongofleva Snura amefunguka kwa kuweka wazi kuhusu madai yanayosambaa kwenye mitandao kuwa anatumia dawa za kutengeneza shepu akisema hajawahi kutumia dawa hizo bali shepu yake ni ya asili.
Akizungumza kwenye kipindi cha ‘Leo Tena’ ya Clouds FM Snura amesisitiza kuwa familia yao imejaaliwa kuwa na shepu ambayo ni asili yao akiamini kuwa Mwenyezi Mungu amewaumba watu kwa utashi wake.
“Kuhusu suala la mimi kutumia Mchina, natamani sana siku moja nije na familia yangu muione. Hii ni asili yetu. Kwetu sote tumejaaliwa na mimi kama Muislamu naapa kwa Mwenyezi Mungu kuwa sijawahi kutumia dawa kuongeza makalio.
“Kama nimewahi, Mwenyezi Mungu anilaani na aondoe Baraka kwenye familia yangu. Sitoweza kupita nyumba hadi nyumba kuwaaminisha watu juu ya hili, ila nikinenepa kila kitu kwenye mwili wangu kinaongezeka.
“Mimi naamini kwamba, kila binadamu ameumbwa kutokana na majaaliwa ya Mwenyezi Mungu pasipokuangalia makabila. Ndio maana wapo Wachaga wenye shepu zao.” – Snura
Aidha, Snura amesema anatamani kuolewa na mwanaume mwenye hofu ya Mwenyezi Mungu akiamini itakuwa rahisi kumfanya naye kuwa kwenye misingi ya Dini ambaye pia atajali familia yake: “Mimi sijawahi kuolewa, nimezaa tu. Nahitaji mwanaume mwenye Imani atakayeijali familia yangu.” – Snura.
Source: Udaku