Staa mwenye umbo na muonekano wa ‘kokoro’, Jacqueline Wolper Massawe ‘Gambe’ amekiri kuwa hakuna msanii wa kike anayeongoza kwa kuhongwa vitu vya thamani na gharama kubwa zaidi yake, Ijumaa tunakutiririshia aya zake.
Jumatatu ya wiki hii, ‘mbayuwayu’ wetu walipiga hodi na kuweka kambi ya muda nyumbani kwake, Kinondoni, Mkwajuni jijini Dar na ‘kumbananisha ukutani’ kwa maswali magumu ambapo pamoja na mambo mengine, alikiri kuhongwa vitu mbalimbali na vigogo, wakiwemo viongozi wa ngazi za juu serikalini pamoja na wafanyabiashara. Wolper amesema japo kuna wasanii wengi wanaohongwa vizuri, lakini yeye amekuwa wa tofauti, kufuatia aina ya vitu anavyopewa ambavyo ni mijengo ya maana na magari ya kifahari.
ALISEMA;
“Naweza kuwa kinara wa mastaa wa Bongo kuhongwa mali na fedha nyingi kuliko msanii mwingine yeyote, kama nyumba, magari lakini kwenye duka hili hakuna mkono wa mwanaume isipokuwa ni jitihada binafsi. “Kama mtakuwa na kumbukumbu nzuri, mtakuwa mnajua habari ya lile gari la kifahari, Toyota Prado nililowahi kuhongwa na mmoja wa wanaume niliyewahi kutoka naye kimapenzi, thamani yangu ni kubwa, mwanaume akitaka kunitokea na kunihonga lazima aje kwa kujitosheleza kikubwa zaidi na ajipange kiume kwelikweli.
” Pia Wolper aliweka wazi kuwa, kwa sasa amebadili mfumo mzima wa maisha yake, ambapo ameachana na utegemezi wa kuhongwa na wanaume ndiyo maana ameamua kujiingiza kwenye ujasiriamali ili atumie jasho lake halisi.
Aliongeza:
“ Hao watu wanaozusha maneno kwamba biashara yangu nimehongwa, huko ni kutafuta kiki na cheap popularity (umaarufu wa bei nafuu) kupitia mgongo wangu, biashara hii imenichukua zaidi ya miaka miwili kuifanikisha, watu waache maneno na badala yake wafanye kazi.
” TUGEUZE SHINGO KIDOGO
Kumbukumbu zinaonesha kuwa, kipindi cha nyuma msanii huyo aliwahi kuhongwa gari aina ya Toyota Prado na aliyewahi kuwa mpenzi wake, Dallas ikiwemo kuishi kwa mbwembwe za kuonesha jeuri ya fedha.
Source: Udaku