Dudu Baya Amshukia Vikali Mwanaye.


Msanii mkongwe wa muziki Bongo, Dudu Baya amefunguka maneno mazito dhidi ya mwanaye Wille ambaye anadai amekataa shule.

Dudu Baya amesema mtoto huyo amekataa shule na kuanza muziki kwa kificho na amekuwa akikutana na baadhi ya wasanii kama Dully Sykes Coco Beach na kuwaeleza dhamira yake ya kuanza muziki lakini hajawahi kumuambia suala hilo.

Dudu Baya ameendelea kusema Wille amekuwa hivyo baada ya kuamia kwa mama yake na kuonya kuwa aendelee na anayofanya ila yeye hawezi kumtafuta.

“Mungu mwenyewe alisema mtoto mwenye busara na hekima humfurahisha babaye lakini na toto jinga, shenzi na pumbavu ni mzigo kwa mama,” Dudu Baya

“Mara nyingi watoto wa namna hii, vibaka, wezi, chagudoa, mashoga wanakaaga sana na mama zao lakini baba yoyote mtoto wa namna hiyo hawezi kukaa naye, huwa wanaitimua ndio maana mtoto anaweza kuwa kibaka mwizi akapelekwa jela baba yake asiende kumuangali lakini mama yake akaenda,” ameongeza.

Dudu Baya amemaliza kwa kusema yeye hamtafuti Wille kwani ni kijana mkubwa mwenye umri wa kati ya miaka 16/17.

Source: Udaku.

Facebook Notice for EU! You need to login to view and post FB Comments!