Staa wa Bongofleva Nay wa Mitego alifika katika ofisi za Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo zilizopo Dodoma kwa ajili ya kuonana na kufanya mazungumzo na Waziri Dr. Harrison Mwakyembe ikiwa ni siku kadhaa zimepita tangu msanii huyo kuachiwa huru.
Nay wa Mitego alikuwa akishikiliwa na Jeshi la Polisi Dar es Salaam kwa tuhuma za wimbo wake wa ‘WAPO’ kudaiwa kutokuwa na maadili kisha baadae aliachiwa huru baada ya agizo la Rais Magufuli kupitia  Mwakyembe ambapo aliomba aonane na Nay wa Mitego ili kumshauri vitu vya kuongeza kwenye wimbo wake wa ‘WAPO’.
Source: Millard ayo