UKWELI KUHUSU WIZI KWENYE BASI LA TOUR YA DRAKE SUMMER SIXTEEN.

 Unakumbuka ile stori ya Drake kuonekana kukasirishwa sana baada vitu vya thamani kuibiwa kwenye basi? Ishu nyingine ni kwamba Dereva ambaye alikuwa akiendesha gari hilo alimshuhudia mwizi akiiba.

Ile Stori ya yule jamaa alieamua kuingia katika basi la Tour ya Drake ya Summer Sixteen inasemakana kwamba Dereva wa basi hilo alimshuhudia mwizi huyo na kusema kwamba wakati anaingia kwenye gari hilo jamaa hakuonyesha wasi, naye akadhani kwamba ni moja ya marafiki wa Drake, Kingine ni kwamba Dereva huyo akufunga mlango wa basi hilo ndipo jamaa aliingia na kufanya wizi wa dola milioni 3 ambazo zimetokana na vito vya thamani vya Dj wa Drake na Future the prince.

Kizuri ni kwamba mwizi huyo hakuweza kusurvive, baada ya muda mfupi alikuwa mikononi mwa Polisi, kupitia video ambayo ilirekodiwa na Tmz ikimwonyesha Drake akiwajibu waandishi kwamba yeye Hakuibiwa kitu chochote kutokana na mabasi hayo kuwa tofautitofauti.

Story by:@Joplus_

Source: Perfect255.com