KEVIN HART AIONGOZA LIST YA WACHEKESHAJI WALIONGIZA MKWANJA MREFU KWA MWAKA 2016 KWENYE JARIDA LA FORBES.

Muigizaji wa Mrekani, Kevin Hart ameongoza orodha mpya ya jarida la Forbes ya wachekeshaji walioingiza pesa ndefu zaidi 2016.

Kevin Hart amefanikiwa kumtoa Jerry Seinfeld aliyeongoza orodha hiyo Kwa miaka 10 mfululizio, Kutoka mwaka June 2015 hadi June 2016 Hart ameingiza dola Million 84.

kevin-hart

Mapato mengi aliyoingiza yakitoka kwenye dili na matangazo, Ziara yake ‘What now Tour’ na filamu kama Central Intellegence na Secret life of pets, Pia ameshika namba 6 kwenye orodha ya mastaa 100 wanaongiza mkwanja mrefu zaidi 2016.

Tazama orodha kamili,

1) Kevin Hart ($87.5 million)

2) Jerry Seinfeld ($43.5 million)

3) Terry Fator ($21 million)

4) Amy Schumer ($17 million)

5) Jeff Dunham ($13.5 million)

6) Dave Chappelle ($13 million)

7) Jim Gaffigan ($12.5 million)

8) Gabriel Iglesias ($9.5 million)

9) Russell Peters ($9 million)

10) John Bishop ($7 million).

Story By: @Joplus_

Source: Perfect255.com