Ujumbe wa Naibu Waziri Kigwangalla kwa Ray C

Naibu Waziri wa Afya Dr. Hamisi Kigwangalla leo Aprill 27 kupitia ukurasa wake wa Instagram amempongeza msani wa Bongo Fleva Rehema Chalamila ‘Ray C’ baada ya kuguswa na wimbo wake Unanimaliza.

“Mimi kama Naibu Waziri wa Mambo ya Wanawake, kama balozi wa wanawake na kama Daktari niseme nimefurahishwa na kuvutiwa sana na jitihada anazofanya huyu dada Ray C nimeguswa na wimbo wake wa unanimaliza.

“Nimeona nimuunge mkono kwa kuwaomba wadau wote ambao mmekuwa naye siku zote mfahamu kuwa sasa anahitaji support yetu zaidi kuliko wakati wowote ule. Tumuunge mkono kwa dhati. Mungu atatujaalia kheir kwenye maisha yetu pia.

“Hakuna aliyekamilika sote tuna vipindi vyetu vya kuanguka Na kwa hakika tunahitaji ‘a second chance’ kila siku za maisha yetu! Hakuna anayeweza kujisimamia mwenyewe, sote tunahitaji mtu mmoja wa kutushika mkono na kutunyanyua pindi tunapoanguka.

“Kila la kheir Ndg. Rehema Chalamila. With our support, even the sky is not the limit! Keep on moving, keep on believing.” – Hamisi Kigwangalla.

Source: Millard ayo